Breaking News

KWANINI SIMU YAKO INASTAHILI KUZIMWA IFIKAPO JUNE 16

Kwa nchi ya Tanzania tunajua kabisa ifikapo tarehe 16/06/2016,Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) itazima na kufanya simu zote ambazo zinatumia IMEI ambazo hazijasajiriwa au sio ambazo zipo sokoni au ambazo si halisi basi zitafungiwa.
IMEI ni kifupi cha maneno ya kiingereza yaani International Mobile Equipment Identity (IMEI) ambazo huwa ni tarakimu 15-17 ambazo huwezesha makampuni ya simu kuiona na kuipa uwezo wa kuwasiliana simu yako.
Umuhimu wa IMEI Namba
IMEI namba zina kazi nyingi hasa zinapowekwa kwenye simu yako ila kubwa kabisa ni kwamba imei namba huwezesha makampuni ya simu kuziona na kujua ni simu ipi inafanya kazi,mahala gani na kwa kiasi gani. Namba hizi hutumika hata kukitokea matukio ya uhalifu au upotevu simu ambapo makampuni haya ya simu huweza kuzizima simu au kufatilia ilipo simu ilopotea.
1.Kurudisha simu ilopotea. SIMU ilopotea inaweza kuwa rahisi kuonekana kwenye vifaa maalumu vya TEHEMA hasa kwa kutumia imei number ambazo huwa ni tofauti kwa kila simu na ndio hasa huwezesha kila simu kupata mawasiliano.
2.Sababu za usalama
Pia panapotekea tukio la kiusalama ambalo huhitaji upatikanaji wa simu ya muhusika njia nyepesi ya kujua yupo wapi ni kufatilia mienendo yake hasa kupitia simu yake hivyo kuwa rahisi kwa wana usalama kumpata na kumtia n guvuni mtuhumiwa au kuvuia tukio fulani la kiusalama
3.Kujua soko na minendo ya biashara
Pia kupitia imei namba makampuni ya simu huweza kujua na kufanya tathmini kuhusu upatikanaji na uuzaji wa bidhaa zao kwa maeneo husika.IMEI namba huwajulisha mahala palipo na wateja wengi wengi wa bidhaa husika au palipo na biashara ndogo ya mauzo ya huduma zao hivyo kubadili maamuzi ya kibiashara
Kutokana na ongezeko na matishio ya ujambazi na uhalifu amabyo yanarandana na mabadiliko ya tecknologia,kwa kulijua hilo tuna haja ya kuzizima na kublock kila kifaa ambacho kinatumia imei fake ili kupata wigo wa kufatilia na kujua kila kinachoendelea hasa kwa vifaa ambavyo havina imei ya kweli
Lakini pia kwa kutambua hatari ambayo muhusika wa kutumia simu anaweza kuipata hasa kifaa chake kutumika kwa uhalifu na matumizi mengine mabaya,tunashauri na kusisitiza watu wote wawe tayari kupokea na kuishi ndani ya mfumo mpya wa kutumia imei za kweli
JINSI YA KUBADILI IMEI...............coming soon
Mwinjuma Kimaya, kwa msaada ya mtandao

No comments