TANGA KOSA LAKO NINI:
Eneo la mkoa:
Mkoa una eneo la 27,348 km² na uko Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ukipakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki na mikoa ya Morogoro, Manyara na Kilimanjaro. Mpaka upande wa kusini unafuata mto wa Mligaji. Mkoa wa Tanga unaunganisha sehemu za pwani pamoja na milima ya ndani kama Usambara.
Kuna wilaya 10 ambazo ni Handeni Vijijini, Handeni Mjini, Kilindi, Korogwe Vijijini, Korogwe Mjini, Lushoto, Mkinga, Muheza, Pangani na Tanga Mjini. Eneo linalofaa kwa kilimo ni 17,000 km². Tanga ni kati ya mikoa midogo ya Tanzania ikiwa na msongamano mkubwa wa wakazi ndani ya eneo lake.
Wakazi
Makabila makubwa mkoani Tanga ni Wasambaa, Wazigua, Wabondei na Wadigo. Wasambaa ndio kabila kubwa lililoko katika milimani ya Usambara, Muheza, Korogwe na Lushoto. Kwa jumla ndio asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa.
Msongamano wa wakazi ni mkubwa hasa wilaya ya Lushoto penye ardhi yenye rutuba nzuri. Wiyala ya handeni kuna machimbo ya madini,ila kuhusu elimu ipo nyuma sana kwani mpaka sasa hakuna shule ya sekondari inayotoa huduma ya kidato cha tano na sita kama haitoshi shule za watu binafsi hakuna hata moja kwa wilaya nzima ya handeni.
Hali ya hewa
Kwa jumla hali ya hewa ni joto lenye unyevu. Handeni kuna joto ikiwa pakavu zaidi. Milima ya Usambara hapana joto sana. Miezi ya Desemba - Machi halijoto huko Tanga inafikia sentigredi 30-32 mchana na 26-29 usiku. Wakati wa Mei hadi Oktoba halijota inapoa ni sentigredi 23-28 mchana na 20-24 usiku. Unyevu iko juu kati ya asilimia 100 na asilimia 65.Maeneo mengi ya mkoa hupokea angalau milimita 750 za mvua kwa mwaka au zaidi. Pwani ni zaidi takriban milimita 1,100 hadi 1,400 mm ikipungua sehemu za ndani isipokuwa milima ya Usambara ambako mvua inaweza kuzidi milimita 2000 kwa mwaka. Uchumi.
Wakazi wengi hutegemea kilimo cha riziki pamoja na ufugaji na uvuvi. Mazao ya chakula hasa ni mahindi, muhogo, ndizi, maharagwe na mpunga. Mazao ya biashara ni katani, pamba, kahawa, chai, nazi, tumbaku na korosho.
Utalii umeanza kupanuka kidogo hasa katika eneo la Pangani,Mapango ya Amboni na kituo cha Makumbusho URITHI Tanga.
Katani ilikuwa zao la biashara hasa kwa ajili ya Tanga tangu kuingizwa kutoka Mexico zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hulimwa kote mkoani isipokuwa Lushoto, hasa Muheza na Korogwe kwenye mashamba makubwa. Mashamba haya yalikuwa ya walowezi, yalitaifishwa baada ya uhuru. Tangu kuanguka kwa sekta ya umma yamebinafsishwa tena siku hizi. Zao la katani inategemea sana soko la dunia, umuhimu wake ilirudi nyuma tangu miaka ya 1960.
Tanga ilikuwa na viwanda vingi kiasi katika miaka ya 1960 na 1970 lakini karibu vyote vimekwama kutokana na siasa ya Ujamaa na uchumi wake ulioiga mfumo wa nchi za kisoshalisti. Viwanda vichache vilivyobaki havizalishi mali kulingana na uwezo wao. kilichobaki hasa ni kiwanda cha saruji Tanga.
Viwanda hizi vilizalisha na kutengeneza ajira nyingi kwa wazawa na hata wa maeneo ya jirani na moa huu.Kutokana na umuhimu wa viwanda hivi na pamoja na ustawi wake kwa watu wa tanga na tanzania kwa ujumla,natumai ni muda wa serikali na mashirika binafsi kufufua na kuendekleza viwanda vilivyokuwa ndani ya mkoa wa tanga.
Viwanda kama vya matunda pale korogwe,viwanda vya chuma pamoja na viwanda vya plastiki pale tanga mjini ni kielelezo tosha cha ustawi na ubora wa sekta ya viwanda kwa mkoa wa Tanga. Ni imani yangu kwamba kipindi hiki cha hapa kzi tu kitaliona nakuliendeleza hili ili kuupa hadhi ya kimkoa mkoa wa tanga na vitongoji vyake.
Pamoja na yote nimekuwa nikitafakari na kujiuliza hasa tatizo la kimaendeleo kwa mkoa wa tanga, nimekuwa nikitafakari na kujiuliza hasa nani chanzo cha matatizo haya na je ni nani atakuwa suruhisho la kudumu la kimaendeleo ndani ya moyo wa maisha yangu. Nina imani na fikra mpya za kimaendeleo na harakati madhubuti za kupelekea kufikisha mikakati ya maendeleo kwa mkoa wa Tanga.
Mwinjuma Kimaya,
Kwa msaada wa mtandao

No comments