DIAMOND NA ALI KIBA: MNAENDA KUIZIKA RASMI BONGO FLEVA
DIAMOND NA ALI KIBA: MNAENDA KUIZIKA RASMI BONGO FLEVA:
Na Mwinjuma Kimaya
#Kila ninapo tazama hali na mwenendo wa tasnia ya muziki wetu wa kizazi kipya kwa miaka 5 ilopita.....utaona ni majina mawili makubwa yaloweza kutulia na kukaa kwenye kilele cha mafanikio kwa miaka yote hiyo.
Hapa naongelea wana muziki wenye mafanikio makubwa kwa miaka 5 mfululizo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na si wengine bali ni Naseed Abdul maarufu kama Diamond Platnumz (Simba) na Ali Kiba unaweza muita King Kiba.
#Hawa watu wana sifa na kariba ya mafanikio......wana maono na fikra za kuifanya Bongo fleva kama mziki wa Dunia.....wana dhamira na moyo wa kufanya mambo ya tofaut kila siku.
ukitaka kipaji na sauti ya kimziki basi utamtaja Ali Kiba lakin pia kama unaguswa na mtu anojituma na kuhitaj kuwa mpya kila siku basi ni Diamond.
#Pamoja na ubunifu wao.....umaarufu wao na uwezo wa kufanya matamasha mahala popote na maonyesho yakafana......
#kwangu nawaona kama watu waloishika Bongo fleva kwa sasa.....watu ambao muziki wa kizazi kipya unawatizama wao watakachofanya...watu ambao wametengeneza makundi makubwa ya mashabiki ambao kila upande una muona mwingine kama hajui anachofanya.
#Makundi haya makuu mawili yamefanya muziki wetu utegemee kwenye aina mbili tu za muziki yaani ule wa Simba au ule wa King...
nnaposema muziki unategemea makundi haya mawili namaanisha kuwa watanzania wamekuwa wakibagua au kuacha kufatilia wana muzik wengine bali wamejikita kwenye kufatilia na kujua mziki wa Diamond na Ali Kiba pekee.
#Hii inafanya Bongo fleva kuwa ni ya watu wawili.....na jamii imekataa kutengeneza mastaa wengine wakubwa sababu ya uwepo wa makundi haya mawili....jamii haitaki kutanua wigo na kuwa na mastaa wengi zaidi ya hawa kama wanachofanya wenzetu wa Nigeria na Ghana au Afrika kusini bali tumeshikilia watu hawa hawa.
#Muziki wetu utakuja kufa na kurudi tulipokuwa siku tukiwakosa hawa watu......tutakuwa wageni wa fursa siku hawa watu wakiamua kuachia muziki huu.....tutahitaji kumtengeneza mastaa mwingine ili waje angalau kufikia mafanikio walofikia hawa watu.......muda tutakao tumia kufanya haya yote ndo muda ambao Bongo fleva yetu itakuwa kaburini ikihitaji wasanii wapya wenye kariba ya Diamond au Ali Kiba.
#Chukua mfano wa Bongo Movie ambayo ilikuwa inategemea uwepo wa Kanumba kuibeba na kuitangaza.....utazame na kuuangalia muziki wa Taarabu mara baada ya mfalme Mzee Yusufu kuachana na kuimba muziki huo.......hawa watu walipoondoka au kukosekana kwenye tasnia husika sote tunajua nini kilitokea.
tusikubali kufika kule, msingi walotengeneza ndugu zangu hawa yaani Kiba na Diamond unapaswa kuwa ni wa jengo lefu la mafanikio. Tutengeneze watu zaidi wenye kuweza kuitangaza vyema nchi na tusiwategemee Diamond na Kiba pekee mana watakuja uzika rasmi mziki wetu siku wakiacha kufanya mziki huu kwa sababu yeyote ile...ama siku wakiamua kustaafu mziki huu kwa malengo yeyote ya mziki au kimaisha.
#mana kwa sasa hawa ndo roho na maisha ya Bongo fleva...roho ikikatika tunajua mwili unakosa kazi na kupelekea kifo cha tasnia husika.....wametubeba kama Taifa ni muda wa kuwapokea mzigo huu mzito na kusimika wengine wengi zaidi ili tusiwe na presha yabkushuka hata tukiwakosa.
#Ni mimi mwananchi wa kawaida.
Mwinjuma Kimaya
0719 88051
No comments