SINGIDA UNITED: INAPOZIVUA NGUO SIMBA NA YANGA SC KIBIASHARA.
Na Mwinjuma Kimaya
#Wakati napata wasaa wa kupitia usajiri ulofanyika leo kwenye vilabu vya hapa nchini, nikakutana na usajiri mkubwa wa aina mbili kwa wachezaji walowahi chezea simba sc wote yaani Ibrahimu Ajibu alieenda Yanga Sc na Pastoey Athanas alitimkia Singida United.
#Niendelee kupongeza usajiri wa vilabu vyote hasa vyenye lengo la kujiimalisha kwa ajiri ya msimu ujao wa ligi ila kwa hili natamani mjifunze kitu hapa.
#Kikubwa leo ulikuwa ni utambulisho wa wachezaji hawa wawili yaani Ajibu alieenda Yanga sc pamoja na Athanas aliyekimbilia Singida United, lakini ukitazama kwa makini mazingira na mahala palipotumika kuwatambulisha wachezaji husika utagundua hiki ninachoenda kukisema.
#Singida United wamemtambulisha mchezaji wao mahala tulivu huku nyuma pakiwa na logo na utambulisho wa makampuni mbali mbali ambayo nna hakika ni washirika wao na wanapata faida ya kuwatangazia brand zao. Pale nimeona makampuni zaidi ya 10 ikiwemo Sportpesa, Puma, NMB, Halotel, Oryxn.k. Hiki walichofanya sio tu wamefanikiwa bali ndivyo hata club kubwa za barani ulaya wanafanya.
#Turudi kwa Yanga Afrika SC, wenyewe hawakuwa na mawazo ya kibiashara, wamemtambulisha Ajibu mahala pasipo rasmi nadhani ni kichumba tu kile huku ukutani palikuwa na rangi nyeupe pekee yaani hata nembo ya Sportpesa ama Quality Group haikuwepo kwenye utambulisho wa Ajibu. Hiki pia kilitokea kwenye utambulisho wa John Bocco pale Simba SC wiki kadhaa nyuma.
#Sitaki kusema namna ya kuboresha mapato hasa kwa matukioa madogo kama hayo ya utambulisha, ntaongea siku ingine bali ningependa kusisitiza kuwa Yanga na Simba SC mna wajibu wa kujifunza kupitia Singida United juu ya malengo ya kibiashara kupitia nembo za vilabu vyenu.
#Na Mwinjuma Kimaya
0719 880514
No comments