Breaking News

UTALII WETU: HII FURSA IMETUPITAJE TANZANIA?


Na Mwinjuma Kimaya

Miongoni mwa mataifa yalojaaliwa na kubalikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii hapa Afrika kama sio duniani ni taifa la Tanzania.

Tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kujisifia juu ya maliasili zetu pamoja na vivutio vingine. Tuna mlima mrefu Afrika, mbuga kubwa za wanyama kama Ngorongoro, Mikumi, Serengeti, Tarangire n.k, tuna fukwe nzuri za kuvutia, bado tuna kreta bila kusahau palipogundulika binadamu wa kwanza pale Olduvai George. Hakika hii ni zaidi ya kutunukiwa.

Pamoja na yote hayo tumekuwa na utangazaji mdogo ama ulokosa uendelevu kuhusu vivutio vyetu. Ijapokuwa sitaacha kupongeza zile mbao za matangazo kwa ile klabu ya uingereza kuhusu utalii wetu ila bado naona tumekosa fursa ya kujitangaza zaidi.

Hapa karibuni tumepata ugeni mkubwa wa wachezaji na watu maarufu walokuja kutalii hapa nchini, achana na akina Roman Abrahamovic nawaongelea akina David Beckham na familia yake, Mahmoud Sakho, Morgan Sheneiderln aliyeko honeymoon, Victor Wanyama pamoja na Neymar Jr. Hapa watu tulipaswa kuweka mipango mkakati ya kuwatumia kututangaza wakati wapo hapa nchini.

Mfano,  Neymar jr pekee ana follower milioni 125 kwenye mitandao ya facebook, twitter na instagram vile vile David Beckham ana wafuasi milioni 54 kwenye mtandao wa facebook pekee huku Instagram akiwa na followers 38.1Milioni maana yake kama tungeamua kuwatumia hawa watu wawili pekee basi sina shaka tungewafikia watu zaidi ya milioni 210 duniani kote.

Hii ni biashara kwetu na kwao pia, tungekaa tufanye nao biashara, tena sisi tukiwa na lengo la mitandao yao ya kijamii pekee. Pengine serikali ingewapa punguzo kama sio kuwapa offer ya kutembelea vivutio vyetu bure lakini tuwatumie kututangaza.

Mathalani, wakiwa hapa ni lazima wapige picha za ukumbusho na kupost kwenye account zao basi tungehitaji kila picha watakayotuma angalau iseme ama kuandika jina la Tanzania, kama ishara ya upatikanaji wa vivutio husika. Kuweka jina na bendera ya taifa letu kwa watu hawa ingekuwa na maana kubwa sana kwa wale watu wanaowafuata kwenye mitandao ya kijamii na pengine watu zaidi wangehamasika kuja na tungepata mara 10 ya gharama tulizowatolewa wachezaji husika. Hawa watu wangeongeza imani na hamasa zaidi kwa vivutio vyetu.

Naiona mbele yetu ikiwa bora zaidi na pengine haya ni matunda ya ule ubao wa matangazo pale Uingereza. Tuongeze bidii zaidi angalau dunia imeshaanza kututambua.

Tuendelee kupambana na kuielewa zaidi diplomasia ya uchumi kwa ajiri ya Tanzania.

Na Mwinjuma Kimaya
0719 8805

No comments