HUU NI MSIBA WA TAIFA, ACHA TUMSHUKURU MUNGU:
Na Mwinjuma Kimaya
#Kifo ni sehemu ya mamlaka kubwa na ya pekee kwa Mungu wetu, kifo ni mawaidha, kifo ni ishara ya ukuu na utukufu wako BABA, kifo ni njia pekee ya kwenda kuuona uflame wa Mungu lakini pia kifo ni ishara ya upendo mkuu wa Mungu wetu kwa waja wake ndo mana anawaita tena mbinguni.
#Ile ajari ya tar 06/05/17 pale Arusha sio tu imetengeneza huzuni kwa Taifa, sio tu imetuleta pamoja kama nchi, sio tu imegusa mamia na maelfu wa watz bali imeacha kovu na jeraha kubwa la maumivu ndani ya mioyo yetu.
#Tunaposema ahsante Mungu kwa kila jambo, tuna maana ya kuukubali utukufu wako kisha kuishi maisha ulotuagiza.
Ahsante Mungu kwa maana uliwaita nao kwa mapenzi yako wakaitika, ahsante Mungu kwa maana maombi yetu yakafunike roho zao, tunashukuru Allah na kuwaombea uwaweke mahala pema panapostahili.
#Ni wadogo kiumri ila ulisema hapana nawahitaji na ukawachukua wanao, ahsante sana kwa yote.
Nakuomba Mungu wangu uwape nguvu na uvumilivu familia zile zilizoguswa, naomba Mungu ukawe mfariji kwa kila Mtz, Mungu wangu washike wazazi ama walezi wa wale watoto, wape ujasiri na moyo faraja juu yako.
#Mungu wetu anajua na kumpangia kila mmoja kifo chake, tuendelee kumtukuza na kuishi kama alivyoagiza.
Tusali sana mana hatujui siku wala saa ya kuijuliwa kwetu.
#Nasema ahsante MunguðŸ˜ðŸ˜
Mwinjuma Kimaya
0719880514
No comments