Breaking News

KAMA NINGEKUWA RAIS WA CLUB YA SIMBA:




Na Mwinjuma Kimaya

Mapenzi yangu kwa club ya Simba yanafanya niishi na ndoto za kimapinduzi hasa maendeleo, ndoto za mageuzi pamoja na maono ya mbali ya mafanikio. Sina nia leo wala kesho ya kuishi ndani ya ndoto yangu bali naitizima miaka mingi ijayo kama ni nyakati za kutimiza unabii na kuweka alama pale mitaa ya Msimbazi.

Miaka yote Simba sc imejinasibu kama club ya wanachi huku uhalisia ukionyesha ina wapenzi na mashabiki wa kutosha nchini,  naitazama Simba sc kama taasisi kongwe yenye ushawishi na wapenzi wengi sana Tanzania.

Tungefanya yafuatayo:

#Tukitengeneza uwezo  kuitangaza chapa ya club yaani brand tutakuwa tumepiga hatua kwa klabu yetu. Brand awareness ndo kila kitu kwenye sports business industry.

#Nazani ni nyakati za kuongeza wanachama na mashabiki wapya ambao sio tu wataweza toa ada ya 1000 kila mwezi bali wawe na uwezo wa kuchangia club zao kwa hiali,  hii itafanya club ziongeze mtaji. Mfano ukiwa na wanachama laki 5 kisha wote wakatoa 12,000/= tu kwa mwaka maana yake club itapata 6 Bilioni.

#Tungeweka utaratibu wa kuuza tickets za mechi zote za club kwa msimu mzima. Najua hapa kuna changamoto ila kwa kuanzia tungeanza na mechi zote za Dar tuuze tickets kwa mashabiki wetu kulingana na hadhi zao. Naamini wapo wanoweza kununua kuangalia mechi za Simba sc Dar kwa msimu mzima.

#Tuigawe fan base ya club zetu kikanda kisha kila kanda iwe na uwezo na nguvu za mamlaka kwenye mikutano mikuu, pawepo ofisi za kudumu pamoja na uwakilishi hasa kupitia hizi kanda club itakuwa na mamlaka ya kuongeza matawi kila mwanzon mwa msimu hivyo kuongeza mashabiki na wapenzi.

#Kila mkoa kuwe na duka kubwa la vifaa vya michezo toka kwenye club,  ambapo vifaa vitauzwa moja kwa moja na club kupitia ofisi ya mkoa kisha ikaongeza mapato.

#Nazani tuna haja ya kuwagawa mashabiki na wapenzi wetu kulingana na hadhi na michango yao kwenye club. Tuwe na aina 3 tofauti ya wanachama yaani wale wa KAWAIDA, VIP A na B kulingana na michango yao kwenye club.

#Kila kwenye Simba day tutatoa nishani kwa wanachama walojitoa na kuipambania club kwa hali na mali hasa kwa utaratibu maalum utakaowekwa huku ukihusisha wanachama wa kila ngazi.

 #Club ingetafuta wadhamini hasa wamatangazo ya biashara zao ambao wangezamini kuanzia vifaa vya mazoezi,  usafiri, kambi,  pamoja malazi ya wachezaji. Hii ningeifanya kwa umakini kupitia kamati ya masoko na mtaji.

#Kama tukifanikiwa kuingiza wastani wa 10 Bilioni kwa mwaka,  basi ndani ya misimu miwili club itafanikiwa kujiendesha kisasa pamoja na kuwa na uwanja wake wa mazoezi ikiwezekana sports center kubwa A. mashariki na kati.

#Ningekuwa na mikutano mikubwa na ziara kwa ajiri ya kukukatana na wadau wa club kila kanda hususani vyuoni kwenye mikoa husika ambapo mara nyingi huku fikra na mawazo mapya ya mafanikio huzaliwa huku.

#Tungeajiri na kushirikisha wataalamu wa kada mbali mbali wenye mapenzi na huruma kwa club katika kila hatua ya maendeleo. Mfano, tukiachana watumishi wanotakiwa na TFF, kamati tendaji pia ningeajiri na kuwa kamati ya masoko, uchumi, TEHAMA, hamasa,  kusaka vipaji pamoja na ile ushauri binafsi juu ya club.

#Ningeweka utaratibu wa kuwasainisha mikataba mirefu ama kuongeza mkataba juu ya mkataba kama njia rahisi ya kutunza wachezaji wetu hii ingeweza zaa biashara ya kuuza wachezaji pia.

#Kila mchezaji tulomkuza tungeweka nafasi kwenye mikataba yao ya kufaidika na ukuzaji wao. Hii ingesaidia hata mchezaji akimaliza mkataba basi aendako kuna chochote tungepata kama Simba SC.

#Naishia hapa kwa leo, Tukutane kwenye wasaa mwingine.

Ahsanteni sana. Ila inabaki pale pale kama ningekuwa Rais wa club ya Simba SC:

#Simba SC Nguvu moja.

Mwinjuma Kimaya
0719880514

No comments