Breaking News

UKIMYA WETU UMEWAPONZA WAKINA ROMA:





Na Mwinjuma Kimaya

#Kwanza nianze na masikitiko makubwa nilonayo juu ya kupotea na kutokuonekana kwa wasanii kama Roma,Mone na wengineo kama tukio lilivyolipotiwa juzi.
Kisha tuendelee kulaani na kupaza sauti juu ya jinai hii kwa watanzania hawa.

#Hatukuwa na aina hii ya maisha hapo kabla na wala hatujazoea kuishi kwa hofu na sintofahamu mana Utanzania wetu umejawa na amani, mshikamano, upendo, utu, busara na uvumilivu.
Haya ni maisha mageni ya uovu ambayo tunapaswa kuyalaani siku zote kabla hayajakomaa kwenye jamii yetu.

#Nikirudi kwenye kichwa cha mada, watanzania ni watu wakalimu, wenye roho za kuvumilia matukio, ni watu wastaarabu na wenye hekima sana kiasi kwamba hata matukio yanowaumiza na kuharibu taswira ya jamii yao wamekuwa wakitumia utamaduni ule ule kuyatatua yani kutumia busara na hekima sana kuyatatua. 

#Tumekuwa wakimya sana kwa matukio makubwa yalokuwa yanahitaji nguvu ya jamii lakini bado tulikuwa wakimya na wavumilivu sana, sitaki kuwalaumu wala kujilaumu bali ni Utanzania wetu.
Ukifatilia matukio kama ya kutekwa kwa Dr Ulimboka na kuteswa kisha kutupwa Mabwepande sijajua kama wahusika walipatikana ama la, ukipitia mauaji ya Dr Mvungi japo hili lipo mahakamani ila tulivyolipokea ni kwa mtazamo ule ule, nakumbuka kutekwa kwa Ben wa Saanane miezi 6 ilopita ambapo mpaka sasa hatujui yupo wapi, bado wakina Yericko Nyerere walishaonja kutekwa pia, sasa nikiunganisha na hili la Roma naiona taswira ile ile ya Utanzania wetu kwenye mambo mazito kwa wenzetu hawa.

#Wakati katiba inatoa mamlaka makubwa na nguvu ya kuamua jambo ndani ya nchi kama nguvu ya umma na matakwa ya wananchi wenyewe, lakini pia bado katiba imehitaji kila mwananchi kulindwa na kuheshimiwa utu wake. 
Napata wasaa mwepesi kuona ukimya wetu namna unavyowapa nguvu watu hawa kuendeleza matukio yale yale kila siku, ukimya wetu unaendelea kuwapa nafasi ya kulala na kupotezea pamoja kushindwa kuyafanyia kazi matakwa yetu hasa mamlaka tuloipa haki ya kulinda katiba na utu wetu pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.

#Siku tukiamka kisha tukaacha kukaa kimya kama Taifa kwa mambo yanogusa utu wetu ndo siku ambayo matatizo haya yataisha kisha heshima na hadhi ya utanzania wetu tutairudisha mikononi mwetu.
Hakuna muujiza wa kukomesha haya bali ni kuamua kurudisha heshima na mamlaka kubwa ya wanachi ili watambue haki na wajibu wao kwa nchi yao.

Mwinjuma Kimaya
0719 880514

2 comments:

  1. Nimeipenda makala yako kijana wangu, coz imejaa ukweli mtupu

    ReplyDelete
    Replies
    1. ahsante sana kaka, ni imani yangu tukiendelea kukaa kimya basi wengi watapotea mikononi mwetu. tuko pamoja

      Delete