Breaking News

DARASSA: MUZIKI NI DARASA LA MAFANIKIO YAKO.




Na Mwinjuma Kimaya

#Bado naikumbuka sana nyimbo pendwa kwa Taifa letu kipindi cha mwishoni mwa mwaka 2016, nyimbo ya hip hop ilotokea kupendwa na kila rika, nyimbo ilowakosha wanawake na wanaume, nyimbo ilopata air time kubwa kuliko nyimbo yeyote kwa mwezi mzima wa 12 kipindi kile. Hii ilikuwa ni nyimbo ya Taifa kwa wakati ule, inaitwa MUZIKI iloyoimbwa na Darasa.

#Naweza sema ndo wimbo pekee wenye mafanikio ndani na nje ya nchi kwa msanii huyu, wimbo uloweza kupenya vyema masikioni mwa wapenda burudani toka kwa mwana hip hop, wimbo wenye view milioni 6 kwake, hajawahi fika hapa toka aanze muziki. Hii ni zaidi ya mafanikio kwake Darasa.
Mana ukiangalia wimbo kama SIKATI TAMAA una view laki 1 pekee hadi sasa hvi ukiwa umetoka zaid ya mwaka 1 ulopita. Darasa hii ilikuwa njia sahihi ya mafanikio yako.

#Wakati nna matumaini makubwa kwa Darasa kuweza kutumia fursa hii ya Muziki kuweza kutoa nyimbo nyingi za maana kwa mashabiki wake, wakati bado natarajia Darasa atumie kukubalika huku kama daraja la kupiga matamasha mengi mfululizo kila mahala hapa nchini, bado nilikuwa nawaza kupitia muziki Darasa angeweza kutafuta Collabo za maana nje ya nchi lakini pia nilikuwa nataraji kupitia muziki darasa angefanya matamasha makubwa hata ndani ya Afrika mashariki, Ila matarajio yangu yakamezwa na ukimya wake, hakuwa amefanya hivo wala kutumia mwanya huu wa kukubalika kama ishara ya mafanikio yake.

#Darasa ghafla akawa kimya, toka matamasha ya mwaka mpya sikusikia promo ya tamasha lake lolote. Darasa umekaa kimya sana na taratibu wadau wanakusahau, unayakimbia mafanikio ambayo tayari yalisha kuwa mikononi mwako. Darasa nilitarijia ile aina yako ya kutoa nyimbo zaidi ya 2 kwa wakati mmoja ingeendelea, sasa hivi upo kimya na sijui unawaza nini.

#Muziki bado unakuhitaji sana, na nafasi bado unayo, wadau bado wanakuhitaji kufanikisha hili, rudi uchukue nafasi yako. Tanzania ilishakubali aina yako ya muziki hivyo kukaa kimya ni kuyakataa mafanikio yako lakini pia ni kutokujifunza wala kupata Darasa kupitia Muziki wako.

#Siku zote kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua bali haja ya mtu ikipatikana ni mti wa uzima.

Mwinjuma Kimaya
07198805



No comments