Breaking News

NAPE: UNAMUHITAJI LOWASSA


  NAPE: UNAMUHITAJI LOWASSA KIPINDI HIKI:


Na Mwinjuma Kimaya

#Wakati napitia matukio makubwa ya jana hasa lile la alokuwa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo mh Nape Nnauye, niliona makosa mengi sana ya kiusalama pale, nliona ukosefu mkubwa wa weredi kwa watumishi wetu wa ulinzi na usalama lakini pia niliona masikitiko na maumivu ya kutokuamini kile anachofanyiwa kama ni kweli yeye mh Nape ndo kinamtokea.

#Ni imani yangu kuwa haikuwa siku nzuri hata kidogo kwake, ilikuwa siku ya kujifunza upande wa pili wa siasa, siku ngumu yenge kujaa dhiaka na dharau kwa yale alopigania ndani ya chama chake, haikuwa siku pengine alowahi kuwaza kama inaweza kuja kutokea kwake ukilinganisha na aloyofanya ndani ya chama chake.

Ni matukio tulozoea yawatokee wanasiasa wa upinzani, labda hajawahi fikiria kama linaweza kuja kumkuta na yeye siku moja. Ila kwenye siasa lolote linaweza kutoka nami namtia nguvu mh Nape, hiyo ndo siasa ya mageuzi.
Tulizoea haya yawakute ndugu zangu akina Lissu, Lema, Mbowe, Lowassa, Waitara na wengineo wenye kariba ya upinzani. Ila kwa yeye imekuwa kama surprise.

#Rai Yangu:
Nape wewe ni mwanasiasa tena ulokomaa kiuongozi, zao la uvccm, umepikwa kinadharia na vitendo kwenye siasa,  nnachotegemea sasa hivi unapaswa kuwa mtulivu kuliko wakati wowote ule, unapaswa kuwa mkimya mwenye kuwaza mbele yako kuliko kipindi chochote cha maisha yako ya siasa, unahitaji kuwa na imani na moyo wa kutambua Mungu yupo nawe.

Unahitaji kujifunza aina ya siasa anazofanya mzee Lowasa, siasa zisizo na kelele ila zenye malengo makubwa ya kuteka hisia za jamii, siasa za ukimya zenye busara maamuzi, siasa zenye mlengo wa kuifanya jamii ijutie kukosa kwenye nafasi husika.
Siasa za kuwasamehe wote walokukosea kisha ujifunze kusonga mbele, siasa za kutokuwapa nafasi maadui zako wajue fikra za future yako.

#Mzee Lowasa anaweza kuwa mwalimu mzuri sana wa siasa za kileo, siasa za karne ya 21, siasa zenye mrengo bora wa kufanikiwa. Nape jaribu kupita njia za huyu mzee anajua mengi na atakusaidia kwa hapa ulipo.

Mwinjuma Kimaya
0719880514

No comments