Breaking News

HARMORAPA: UNAJUA KUZIISHI NYAKATI ZA MUZIKI WAKO



#HARMORAPA: UNAJUA KUZIISHI NYAKATI KWA MUZIKI WAKO:

Na Mwinjuma Kimaya

#Pamoja na umaarufu aloupata kwa wakati mfupi toka nimtambue rasmi.....sikuwa na shauku wala hamasa kubwa ya kumzungumzia kijana machachari, ingizo jipya, mtu wa furasa za matukio yaani #Harmorapa.

#Alianza kama masiala hasa kujifananisha na moja kati ya wasanii wa WCB ambaye kwake alikuwa ni kama ana mkubali na kuelewa kazi na muonekano wake.....pamoja na kusimangwa huku watu wengi wakimkosoa bado alisimama pale anapopaamini......alipigania muziki wake huku aliendelea kujitambulisha kama msanii nguli wa kizazi kipya.

#Wakati napata taarifa ya kusikitisha juu ya kile ule uvamizi wa kituo cha habari cha Clouds na moja kati ya viongozi wa juu wa mkoa wa Dar.......niliona salamu za pole pamoja maandiko ya kulaani kile kilichotokea siku ya jana toka sehemu tofauti tofauti....toka mahala na kwa wadau tofauti tofauti ndani na nje ya Taifa.
Ila niliona kitu cha tofauti kabisa toka kwa msanii #Harmorapa......wakati wasanii wengi wakiwa kimya juu ya tukio lile hata kwa kupost tu...yeye alifunga safari hadi Clouds Media kisha akawapa pole na masikiriko yake kwa kilichotokea.

#Kwangu niliona strategy muhimu kwake huyu kijana....nliona namna anavyoweza kucheza na upepo wowote wa burudani ambao utamfanya aendelee kuzungumzwa na wadau wa tasnia ya muziki......nimeng'amua uwezo wake wa kuishi kulingana na nyakati hasa matukio makubwa yanoweza mpa nafasi ya kuonekana.
nikikumbuka alivyompigia magoti Ally Kiba......alivyoenda Central kuhakikisha kama jina lake halipo kwenye list ya mkuu wa mkoa...achana na kupiga kwake picha na wasanii maarufu...bado sijasahau baadhi ya mistari ya wimbo wake....ni msanii ambaye anaweza tengeneza habari zake muda wote na kumfanya watu wajue yupo.

#Muda mwingine muziki wetu unahitaji ubunifu na aina tofauti ya kufanya watu wajue upo......kulingana na kariba yake imetokea sasa hvi watu wameanza kufatilia kazi zake.....watu wameanza taratibu kumuelewa hasa nyimbo yake ya "Kiboko wa mabishoo". #Hongera kwake na kwa uongozi wake kwa kuzijua nyakati na kuishi kulingana na nguvu za mitandao ya kijamii.

#Mwinjuma Kimaya
 0719880514

No comments