Breaking News

#NAMUHITAJI WEMA SEPETU


:


Na Mwinjuma Kimaya

#Yes, namuhitaji Wema Sepetu, sijakosea nilichoandika bali nitafafanua mawazo yangu hasa nikilenga biashara na maisha ya kistar.

#Wema Issack Sepetu ni miongoni mwa mastar ambao ndani ya miaka 10 wamekuwa juu na hawajawahi shuka, miongoni mwa celebrity walokaa kwenye kilele cha ustar kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa nembo ya ulimbwende, amekuwa alama ya umaarufu kwa watz, Wema amekuwa icon kubwa hasa kwenye soko la filamu na maisha ya umaarufu.

#Kulingana na umaarufu wake, kutokana na brand alojijengea, kutokana na wigo wa mashabiki alonao, kulingana na hulka na aina ya mashabiki alonao ambao hasa wanapenda na kujari kile anachofanya, Wema chochote anachofanya kinapaswa kuwa biashara, kila analoliishi linapaswa kuwa ni sehemu ya biashara kwa makampuni tofauti tofauti. Wema Sepetu akiamka asubuhi hadi anaenda lala anapaswa kuwa ameishi ndani ya baishara kwa kila kitu cha kawaida alofanya kwa
maisha yake. Hivi ndivyo watu maarufu wanaishi hata kwa wenzetu.

#Mfano, asubuhi akipiga mswaki kisha akapost anatumia whitedent unafikiri watu wangapi watahamasika na bidhaa husika, nani anawaza dada huyu akavaa nguo ya kutokea kisha akasema nimevalishwa na Speshos, ushawaza Wema akiwa na gari kisha ikawa na nembo ya Toyota Tanzania, vipi akionyesha makochi ya sebureni kwake kisha akawatag lifemate furniture, unafikiri saloon yako itakuwa na wateja kiasi gani kama utamrembe kisha akakutag jina lako, unafikiri simu yake Samsung ikionekena hadharani si ni biashara tayari, ile saa pale mkononi, ama urembo wa shingoni utoke Uru labda. Wema anapaswa kila anachofanya kiwe ni kwa ajiri ya brand awareness.

#Huyu dada sio tu anamvuto bali ana ushawishi wa kutosha kwa jamii, ni rahisi kupenya na kuifikia jamii ya kitanzania kama unaweza mfanya Wema Sepetu kuwa balozi wa bidhaa zako. Mtu mwenye wafuasi milioni 2.9 Instagram pekee sio jambo dogo, yani ukimvalisha maana yake bidhaa yako itaonekena na watu zaidi ya milioni 2. Hii ni fursa na hela inayotembea. Wema anahitaji kuishi kibiashara, mana jina lake ni biashara tosha kama ataamua kuishi kibiashara.

#Najua ana ubunifu anaoufanya hasa ile App yake, ila kile amekianza tu anapaswa kuwaza mbali zaidi. Mfano, Wema akawaza kuanzisha Wema Tv kule Youtube kisha akawa anapost maisha yake ya kawaida ya kila siku, uwezo wake wa kufikisha views 50000 kwa kila video kisha akawa na video 20 pekee,anaweza tengeneza zaidi ya milioni 2 kwa kutumia Youtube Adsense, bado matangazo yatamfikia kisha atapata pesa zaidi. Hata ile App ilipaswa kuwa sio tu ya habari zake bali ya kuonyesha matukio yake ya kila siku. Mathalani Wema akatengeneza short film na Diamond, ama Ally Kiba kisha akaiweka Youtube, ama video ya maisha ya kawaida na Mzee Majuto, video ikimuonesha anapika ama anapiga soga na majirani zake, hela ipo kwenye jina la huyu malkia. Ndiyo naiona.

#Nasema na kusisitiza, Namuhitaji Wema Sepetu naweza ongeza kitu kwenye mawazo yake pamoja na uongozi wake.

#Mwambieni, hata hela haijui thamani yake mpaka itakapotumika kufanya yale ya thamani.

Na Mwinjuma Kimaya

No comments