SHILOLE: SHISHIFOOD NI MUHIMU KULIKO UMUHIMU WAKE:
Na Mwinjuma Kimaya
#Shilole, nikitaja jina hilo hapa huwa nataja msanii wa kizazi kipya, muigizaji, mjasiamali, mpambanaji, mtu anayethubutu na kujaribu, mwanamke anojitegemea, mama lishe pamoja na brand kubwa miongoni mwa wapenda burudani.
#Leo nitaongelea Shishifood kama mtoto wa jina la shilole, yaani brand ilozaliwa toka ndani ya jina shilole tukapata shishi kisha tukaleta shishifood.
#Shishifood ni miongoni mwa ubunifu wa wanasanaa wetu ninaoupenda na kuuheshimu sana, kwanini? kwa sababu ni platform ambayo inazalisha huduma na bidhaa ambazo zina mgusa mtanzania wa chini kabisa, yaani yule wa maisha ya kawaida ama maisha ya kati.
#Huu ni mgahawa, ambao unatoa huduma ya chakula tena wanakuletea ulipo.
#Shilole fanya yafuatayo, itakusaidia kwenye biashara yako hii ya mama lishe ikizingatiwa huwezi kupanda kwenye majukwaa ukifikisha umri mkubwa hasa uzee, ila biashara itabaki nawe dada angu:
#Kwanza, lazima ujitofautishe na wauzaji wengine wa chakula hasa online food point ikiwemo #kfc, wale wanatarget watu wenye kipato cha juu ama cha kati, shishifood lazima ishuke kwenda kwenye watu wa kipato cha chini na cha kati ama kuendelea.
Nina maana chakula chako kiweze nunulika angalau kwa bei zetu za sh 1500 hadi 2500 zikiwa na ubora ule ule.
#Pili, kulingana na uhalisia, achana na wazo la kumpelekea mteja chakula, watu wa chini hawawezi zile gharama za usafiri, bali cha kufanya ni kuweka Mobile Restaurants ndani ya dar zenye jina lako yaani shishifood kisha kila penye watu wengi unapeleka chakula na kukiuza pale kikiwa tayari.
Maana yake, utakuwa na vituo tofauti tofauti vya kuuzia chakula chako hususani maeneo ya makazini ikiwemo #kariakoo, #posta, #mbagala, #gongo la mboto, #magomeni, #kimara, #ubungo na kwingineko. Yaani unawafata wateja na kuwalazimisha kula bidhaa zako.
#Nitaelezea mobile restaurants kwa kirefu siku ingine.
#Kila jumapili ya mwisho wa mwezi, unaweza weka mahala mgahawa wako na shishifood event kisha ukawa unauza tickets za taratibu hadi mwezi uishe, utaomba media tour pamoja na njia zingine za kuwafikia watu wako, ikiwemo kuomba mastaa wenzako support waje angalau ile siku ya kwanza. Unaweza chukua order ya kuwalisha watu siku hyo kwa kiasi fulani, mfano 15k milo ya siku nzima kisha wanawaona na kupiga picha na mastaa wa siku husika.
#Chukua tenda ya kupika chakula kwenye sherehe na matukio makubwa makubwa kupitia #shishifood, kisha hakikisha unafanya vyema kwa kila tukio unalopewa uandae chakula cha siku husika.
#Fungua migahawa yako mahala tofauti tofauti mikoani, mfano kwenu Igunga na popote unapohisi una mashabiki wengi wa kutosha, itaongeza thamani ya bidhaa zako pamoja na kipato husika.
#Tafuta wale mama ntilie maarufu hapa mjini, kisha waweke kwenye kampuni yako ili waongeze ujuzi na maarifa ya ipishi zaidi, hii itaongeza thamani ya bidhaa zako.
#MUHIMU
ukiweza kulisha watu 1000 pekee ndani ya Dar nzima kila siku kwa chakula cha shilingi 2000 pekee maaana yake utakuwa umeteneza zaidi ya shilingi milioni #2 kwa siku husika. Maana yake utakuwa umetengeneza shilingi milioni 60 kwa mwezi bilia kutoa gharana na matumizi.
Dada angu kama unaweza ingiza milioni 60 kwa mwezi, nadhani hata kupanda kwenye majukwaa unaweza kuamua kuacha na kujikiti kwenye miradi hii husika.
Miradi inayogusa watu wa chini huwa inalipa sana.
#Na Mwinjuma Kimaya
No comments