Breaking News

KENYA WAMEFANIKIWA, SISI BADO TUNAJIFUNZA:

Na Mwinjuma Kimaya

#Wakati natazama na kufatilia namna kesi ya uchaguzi mkuu kwa majirani zetu Kenya ilivyooendeshwa kisha hukumu ilivyotoka na namna wanachi walivyoopokea hukumu ile, nilipigwa gazi kwa sekunde kadhaa mara baada ya kuhamisha taswira nzima ya Kenya kisha nikaileta kwenye nchi yangu, taswira ya tume yao ya uchaguzi, mchakato wa uchaguzi, nguvu ya mahakama kupokea mashauri ya matokeo hasa yale ya Uraisi ambapo kwetu hatuna hicho kipengele kwenye katiba, nikajikuta natamani tuwe na katiba mpya tena kwa kuanzia tuanze na ile Rasimu ya Jaji Joseph Sinde Warioba.

Nasema katiba kwa maana kila walichofanikisha Wakenya leo, ni jitrahada na mwamko mkubwa ulofanikisha kupatikana kwa katiba yao mpya mwaka 2010, Raila Odinga sio tu ni mwanachama na kiongozi wa upinzani nchini Kenya lakini pia namuita baba wa demokrasia ndani ya Kenya. Odinga amehusika kuiweka taswira ya Kenya kwenye mikono halali ya kidemokrasia, amemlazimisha Uhuru kuishi ndani ya demokrasia, amefanya upinzani uwe na nguvu huku akiweka nguvu na imani ya kuja kushika kiti cha uraisi hapo baadaye kama sio uchaguzi utakaofanyika siku 60 zijazo.

Tuna jambo moja na muhimu la kujifunza kama Taifa, tunahitaji agenda ya kitaifa, mtazamo mpya wa kinchi pamoja na nuru mpya Taifa kwa miaka ijayo. Tunahitaji katiba mpya. Hakuna namna tunaweza fikia viwango bora vya kidemokrasia ikiwa katiba yetu ipo wazi na inategemea maono ya Raisi pekee. Ndugu zangu wanachama wa vyama vya upinzani hakuna namna tunaweza fika kwenye demokrasia kama Kenya ikiwa tuna katiba tulonayo. Katiba yetu ina mapungufu ikiwemo kukataza kuhoji matokeo ya Urais mahala popote, nguvu kubwa ya Rais, tuwe na tume huru ya uchaguzi, mahakama kusimama kama taasisi pamoja na nguvu ya Bunge kuwepo kikatiba.

Kenya wameweza sio kwa bahati mbaya la hasha bali ni kwa kujitolea kuitafuta katiba bora inowafanya wapate haki zao popote ndani ya nchi dhidi ya yeyote, katiba inoheshimu haki za wengine huku demokrasia ikiwa ni lengo kuu la maendeleo yao. Huu ndo msingi wa demokrasia na utawala wa sheria popote pale duniani.

Mwinjuma Kimaya
0719880514

No comments