Breaking News

HAKUNA SABABU YA KUTOKA TENA NJE YA BUNGE


Wakati tukiwa na sintofahamu juu ya wabunge wa upinzani kususia na kutohudhria vikao vyote vya bunge vinavyoendelea na Naibu Spika wa Bunge kwa kile wanachodai kutokuwa na imani na naibu spika huyo wa bunge la jamhuri ya muungano la Tanzania.

Wabunge hawa wa upinzani wameonyesha hasira na mioyo ya kutokuwa na imani na kiti cha spika hasa kikiongozwa na naibu spika kwa sababu wanasema amekuwa akikiuka kanuni za bunge na kuwakandamiza wao au kutowasikiliza kile wanachosema.

Kutoka na kususia vikao vya Bunge sio kuwa ni mara ya kwanza kwa kambi ya upinzani kufanya hivyo bali wamekuwa wakifanya na kutekeleza kususia huko kama njia ya kufikisha mitazamo yao hasa wanapoona wanaonewa na pengine hakuna njia ingine ya kupata haki yao kwa wakati huo.

Tumeona toka kipindi cha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya ambapo walitoka na kususia vikao viliovyobaki hii ikapelekea kuzaliwa na kuasisiwa kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi yaani UKAWA ambapo ni muunganiko wa vyama vikuu vya upinzani nchini.

Lakini kutokana na kutoka kwao huku shughuli za Bunge kuendelea matokeo yake wamekuwa wakipitwa na mijadala ambayo kwa owezo wao lakini kwa mamlaka ya uwakilishi walonayo wangeweza kujadili na kuongeza kitu chenye maslahi kwa Taifa.

Umefika muda sasa kwa wabunge wangu hasa wa upinzani kutafuta namna ya kupambana na kuendeleza mijadala kwa hoja bila kufikia hatua ya kususia vikao kwani kufanya hivyo sio tu kunatunyima haki sisi tulowapa mamlaka ya uwakilishi bali pia imekuwa ni njia ya wao kuonyesha unyonge na kuwapa na nafasi ya kufanya wanachotaka wabunge walobaki.

Mnahitaji mikakati mipya yenye mbinu mahsusi za kupambana na kila hoja inokuja mbele yenu kwani sisi wananchi tumekuwa tukifatilia na kujilizisha nani ni mbunge mwenye kusisimamia maslahi ya nchi na nani yupo kwa ajiri ya manufaa yake.

Kutoka nje ya Bunge siona kama ni suruhu ya mwiba wa hoja za uonevu juu yenu bali mnastahili kupambana kwa hoja mkiwa ndani ya eneo la chumba cha Bunge bila kuuacha uwanja.

Ahsanteni:

Mwinjuma Kimaya

0625 522 322


1 comment: