USIOGOPE KUSHINDWA BALI KIMBIA KUTOKUTHUBUTU:
SAFARI YA UBILIONEA:
Wengi wetu tumekuwa na na matumaini makubwa ya kufanikiwa nakufikia maisha mazuri yenye kariba ya utajiri na kuucha kando umaskini wa kipato.
Wakati tukiwa bize kuukataa na kuukimbia umaskini ni muda ambao tunapambana na kukutana nakila aina ya majaribu, hila na hata vikwazo vikubwa kutoka kwa watu wa karibu yetu.
Maisha yanaenda kasi sana na mtaji wa kujaribu unavuja juu ya miili yetu huku tumaini la kufikia malengo likiwa linazunguka mawazo na mitazamo yetu. Maisha ni mapamabano na uthubutu, kufanikiwa sio tu kunahitaji kujitoa na kupambana na changamoto kwa uhalisia bali unahitaji kuhamasika na kuukataa mfumo wa kimaskini kwako.
Hakika mapambano ya kuusaka ubilionea yanahitaji kutokukata tamaa na wala kushindwa kujaribu.Ikitokea fursa ya kiuchumi unapaswa kujaribu kisha kuthubutu ili kufikia malengo ya maisha yako.
Waliofanikiwa ni watu walokataa kukata tamaa na kupambana kwa uvumilivu kisha maisha marefu ya kuvumilia huzaa matunda ya mafanikio kwao.
Muda ukawe mali ya kufanikiwa kwako, Mapambano ya adui maskini ni vita ya ubilionea dhidi ya tabaka linalohitaji kufika juu kimafanikio.
USIKATE TAMAA KAMWE.........................PAMBANA KILA UKIPATA NAFASI YA KUPIGANIA KILICHO BORA.
HAKIKA SOTE TUTAFANIKIWA KAMA TU MOYO WA UBILIONEA UNAISHI NDANI YETU.
No comments